Tuesday, 23 August 2016


                                      IJUE EAGLE 

Eagle Academy Ilianzishwa mwaka 2000 kutokea kwenye Mgogoro wa Klabu kongwe Maeneo ya Sahare Cabo Delgado.Baadhi ya Wanachama,wapenzi na Wachezaji Wa Delgado kugawanyika kimtazamo na kimfumo Wa Uendeshaji timu hususan maswala ya Utawala.
Viongozi waliokuwa mrengo Wa kushota wakaianzisha timu iliyoitwa Cabo Rangers..Bado Viongozi Wa Cabo Delgado wakasema jina LA Cabo Rangers ni LA kwao na kuwalazimisha walibadilishe na kuondoa neno Cabo.
Uongozi uliokuwepo Cabo Rangers Kwa Wakati huo ndipo Wakabadili Usajili Wa jina Cabo na Kuwa Eagle Rangers.na ilianza kucheza ligi ya wilaya mwaka 2000 Rasmi.
 Baada ya kushiriki ligi ya wilaya Kwa miaka mitatu..Uongozi Rasmi Wa Eagle ambao haukutetereka na mapinduzi na Maneno ya mtaani Uliamua kuanzisha Shule ya Mpira na hii ilichagizwa sana baada ya Mwalimu na kiongozi Wa timu Bakari Shime Kutoka kusomea kozi ya Juu ya Ukocha Wa watoto wadogo inayotambuliwa na Shirikisho LA soka ulaya kutokea Kwa mkufunzi Wa Kiholanzi
Hapo ndipo Kituo hicho kikaanzishwa Rasmi mwaka 2003 kikaitwa Eagle Sports Academy Chini ya mwamvuli wa Youth Soccer and Development Program (Yosotadep)na mwaka 2004  timu zote mbili ziliingizwa kushiriki ligi ya wilaya ya Tanga huku Eagle Rangers ikiwa na Vijana chini ya miaka 17 na wachache waliozidi miaka 17..Wakati Eagle Academy ukiwa na vijana Wa chini ya miaka 15.
Kwa maajabu kabisa timu iliyokuwa na vijana Wa Chini ya miaka 17 Eagle Academy wakafanikiwa kuipandisha timu yao kwenda ligi ya mkoa kinyume na matarajio ya Uongozi mzima Wa Eagle.
 Mpango ulikuwa ni Eagle Rangers Kucheza ligi ya mkoa na Academy ya watoto icheze ligi ya wilaya.ila imefanyika kinyume chake
 Mafanikio .
Kuanzia mwaka 2000 Hadi 2014 Timu imeweza Kwa kila mwaka kufanya Ziara za nje ya mikoa Kwa ajili ya mashindano ya vijana.
Mwaka 2014 Timu ilifanikiwa kutwa ubingwa Wa Africa Mashiriki na kati Wa vijana chini ya miaka 17 Kwa kuwafunga Azam Fc ya Dar.
Timu pia Imeweza kushiriki ligi zinazotambuliwa na Shirikisho LA Mpira Wa Miguu Tanzania Kwa miaka 17 bila kukosa
Martin: Timu pia imeibua vipaji mbalimbali vya Vijana kuchezea ligi kubwa Tanzania bara na Visiwani.
 Huku ikijivunia mafanikio makubwa zaidi ya mkufunzi wao mkuu kuwa Kocha Wa Timu ya Taifa ya Vijana Tanzania hiyo inathibitisha ubora Wa Elimu iliyokuwa inatolewa kituoni.
 Malengo ni Eagle Academy kuja kucheza Ligi KUU bara kabla ya kutimiza miaka 20.

No comments:

Post a Comment